Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP kulinda mazingira olmpiki ya 2014 Sochi

UNEP kulinda mazingira olmpiki ya 2014 Sochi

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kwa ushirikiano na mashirika yanayoandaa mashindano ya olimpiki ya mwaka 2014 yatakayoandaliwa mjini Sochi nchini Urusi wamejitolea kurekebisha uharibifu kwenye bonde la mto mmoja mihimu nchini humo.

Mkurugenzi wa shirika la UNEP Achim Steiner anasema kuwa sababu kuu ambayo imewafanya kushirikiana na kamati ya kimataifa ya olimpiki ni kuwa mashindano ya olimpiki yatatoa fursa ya kuonyesha uvumbuzi na yanachochea kupatika kwa nyakati nzuri za baadaye kitaifa na kimataifa.