DPRK yahitaji dola milioni 1 kukabikli ugonjwa wa miguu na midomo kwa mifugo:FAO

24 Machi 2011

Vifaa na madawa ya takribani dola milioni moja vinahitajika haraka ili kusaidia kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa miguu na midomo kwa mifugo nchini Jamhuri ya watu wa Korea DPRK suala ambalo ni muhimu kwa usalama wa chakula.

Onyo hilo limetolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO ambalo limeongeza kuwa mipango ya muda mrefu pia inahitajika ili kuboresha huduma ya afya ya mifugo nchini humo . FAO na shirika la afya ya mifugo duniani OIE wailizuru DPRK mapema mwezi huu kwa ombi maalumu la serikali.

FAO inasema ugonjwa huo hauna tishio la moja kwa moja kwa afya ya binadamu na umeripotiwa katika majimbo 13 nchini DPRK ambayo yana jumla ya ng'ombe 577,000, nguruwe milioni 2.2 na mbuzi milioni 3.5.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter