Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani wa Indonesia wapongezwa na UM

Walinda amani wa Indonesia wapongezwa na UM

Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa operesheni za kulinda amani Alain Le Roy aliyeko ziarani Indonesia kwa siku tatu amekaribisha mchango unaotolewa na walinda amani wa Indonesia na mipango yao ya baadaye ya kuongeza mchango wao.

Le Roy amesema walinda amani wa Indonesia ni watu wenye ujuzi, wanaojitolea na utendaji wao ni wa hali ya juu. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Jakarta ameongeza kuwa walinda amani hao wanakaribishwa na wenyeji kila wanakotumika kwa niaba ya Umoja wa Mataifa .

Amesema Indonesia ina ari ya kushiriki shughuli za kulinda amani na walinda amani wake wanawasilisha mila za nchi yao, maelewano na ustaarabu wa hali ya juu.