Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IFAD kuisaidia Kenya baada ya kukumbwa na ukame

IFAD kuisaidia Kenya baada ya kukumbwa na ukame

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na maendeleo vijijini atawasili nchini Kenya Jumamosi wiki hii ili kutoa msaada kwa taif hilo la Afrika ya Mashariki ambako watu masikini milioni 2.4 katika maeeneo ya vijijini wanakabiliwa na upungufu wa chakula kutokana na ukame.

Ziara ya Kanayo F, Nwanze raia wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD, inafuatia ripoti iliyotolewa mapema mwezi huu na serikali ya Kenya na washirika wake ikionyesha upungufu wa haraka wa chakula miongoni mwa wakulima.

Ripoti hiyo ilibaini kwamba idadi ya watu wanaohitaji chakula na msaada mwingine imeongezeka kwa asilimia 50 katika kipindi cha miezi sita kutoka watu milioni 1.6 mwezi Agosti 2010 na kufikia watu milioni 2.4 Februari 2011.

Katika ziara yake atakunata na viongozi wa serikali na kujadili masuala ya kuinua kipato cha wakulima wadogowadogo, fursa mpya za biashara vijijini, na kuzuru miradi mbalimbali inayofadhiliwa na IFAD. Tangu 1979 IFAD imewekeza zaidi ya dola milioni 214 kuisaidia juhudi za serikali ya Kenya za kupunguza umasikini vijijini.