Skip to main content

UNESCO imetaka maeneo ya urithi wa kitamaduni Libya yalindwe

UNESCO imetaka maeneo ya urithi wa kitamaduni Libya yalindwe

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova leo ametoa wito kwa serikali ya Libya na muungano wa nchi zinazotekeleza azimio la vikwazo vya anga Libya kuheshimu mkataba wa Hague wa kulinda maeneo ya kitamaduni katika wakati wa vita vya silaha.

Mkataba huo wa 1954 na muongozi wa 1999 unazitak operesheni za kijeshi kuepuka kuharibu maeneo ya kitamaduni. Nchi kumi hadi sasa zimejiunga katika utekelezaji wa azimio hilo la baraza la usalama namba 1973 zikiwemo Ubelgiji, Canada, Denmark, Ufaransa, Italia, Qatar, Hispania, Emarati, Uingereza na Marekani.

Bi Bokova amesema kwa mtazamo wa urithi wa kitamaduni Libya ina umuhimu mkubwa. Amesema kuna maeneo mengi ambayo ni ya kumbukumbu ya historia ya Libya na ni muhimu yakahifadhiwa lakini kuna maeneo matano yaliyoorodheshwa kwenye urithi wa dunia na UNESCO