UM watafuta uvumbuzi kurejesha mazungumzo ya Israel na Palestina

23 Machi 2011

Wakati hali ya mambo ikiendelea kuchacha huko mashariki ya kati ambako kunaripotiwa kuendelea kushamiri kwa vitendo vya uhasama baina ya Israel na Palestina, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa kundi la Quartet kuongeza msukumo ili pande hizo zirejea kwenye mazungumzo ya amani.

Majadiliano ya kusaka amani kwa pande hizo mbili yalivunjika mwaka uliopita kufuatia hatua ya Israel kuendelea na ujenzi wa makazi ya walowezi kwenye ardhi ya Palestina. Msaidizi wa Katibu Mkuu anayehusika na masuala ya siasa Oscar Fernandez-Taranco ameuambia mkutano wa baraza la usalama kuwa lazima kuchukuliwa  hatua za haraka kuyarejesha mazungumzo hayo.

Amesema kuwa Israel imeendelea kujiimarisha na ujenzi wa makazi hayo katika eneo la ukingo wa Gaza, kitendo ambacho kinajenga hatari mpya kwa eneo hilo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter