Taarifa za hali ya hewa duniani ni muhimu sana:WMO

23 Machi 2011

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa , shirika la kimataifa la hali ya hewa duniani WMO limesema kauli mbiu ya mwaka huu ni "tabia nchi kwa ajili yako" hasa kwa kutambua mchango wa idara za kitaifa za hali ya hewa katika maisha ya kila siku ya mwanadamu.

Shirika hilo linasema hali ya hewa siku hizi ni kitu muhimu katika usalama wa maisha ya watu, faida na athari za kiuchumi kwa mataifa yote .

Katibu mkuu wa WMO Michel Jarrud amesema taarifa za wakati za hali ya hewa zitaendelea kuhitajika kwa watoa maamuzi na sekta za kiuchumi na kijamii hasa katika mipango ya kudhibiti athari zinazoweza kusababishwa na kubadilika kwa hali ya hewa.

WMO imesema mfano mwaka jana kumekuwa na matukio tofauti duniani huku Urusi ikikabiliwa na joto kali na sehemu nyingi za Afrika kukumbwa na ukame au mafuriko, na majanga ya asili kama tetemeko Haiti ni ishara ya muhimu wa kujiandaa kwa taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter