Libya yasisitiza kuwa ina akiba ya kutosha ya madawa na chakula na haihitaji msaada wa kimataifa:UM

23 Machi 2011

Serikali ya Libya inasisitiza kwamba ina chakula na akiba ya kutosha ya madawa na hivyo haiitaji msaada wa kimataifa amesema mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa Libya Rashid Khalikov.

Akizungumza mjini Geneva hii leo baada ya kurejea kutoka Libya amesema hata hivyo Umoja wa Mataifa bado unahofia hatma ya raia nchi humo ambao wanabeba athari za machafuko. Amesema Umoja wa Mataifa hauana kituo ndani ya Libya jambo ambalo linafanya kuwa vigumu kwa mashirika yake ya misaada kuendesha shughuli zao.

(SAUTI YA RASHID KHALIKOV)

Bwana Khalikov amesema amezungumza na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na kutekeleza vikwazo vya anga kuhusu umuhimu wa kuwalinda raia na kuhakikisha operesheni zao za kijeshi zinazingatia shirika la kimataifa za haki za binadamu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter