UM wataka uungwaji mkono wa masuala ya amani toka nchi wanachama

22 Machi 2011

Kamishna ya Umoja wa Mataifa inayohusika na ujenzi wa amani inawinda ushawishi toka kwa nchi wanachama wa umoja huo kwa ajili ya kuleta utengamao zaidi katika maeneo ambayo yalitukumbia kwenye vita kwamba isije yakaangukia tena kwenye hali hiyo.

Kulingana na mwenyekiti wa kamishna hiyo aliyemaliza muda wake Peter Wittig amesema kuwa kuna haja kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Mataifa wenyewe kuweka shabaya ya pamoja kuzuia maeneo hayo yaliyokubwa na machafuko yasijirudie tena kwenye hali hiyo kwa kuhakikisha kwamba inaweka kipaumbele kwenye maeneo muhimu.

Kuwepo ushirikiano wa karibu baina ya kamishna ya ujenzi wa amani na makundi mengine ya kiushawishi ikiwemo viongozi wa kisiasa, timu za usakaji amani na jumuiya za maendeleo ni fursa tosha inayoweza kufanikisha azma ya kuzisaidia nchi hizo kutorejelea tena hali ya kale, amesisitiza mwanadiplomasia huyo.

Kamishna hiyo kwa hivi sasa inaangazia zaidi nchi tano zilizopitia machafuko ya kisiasa ambazo ni Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Guinea-Bissau, Liberia na Sierra Leone.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter