Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na viongozi wa Tunisia na kuwapongeza wananchi

Ban akutana na viongozi wa Tunisia na kuwapongeza wananchi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliyeko ziarani Afrika ya Kaskazini leo amekutana na viongozi wa Tunisia mjini Tunis.

Katika mazungumzo yake na Rais Mbazaa, waziri mkuu Essebsi na waziri wa mambo ya nje Kefi Ban amefahamishwa kuhusu mipango ya Tunisia ya njia ya kuelekea demokrasia na kipindi cha mpito.

Ban pia amekutana na wajumbe wa vyama vya kisiasa, na viongozi wa vijana, baadaye leo anatarajiwa kukutana na wawakilishi wa jumuiya za kijamii na kuwafahamisha kuwa amefika Tunisia kuwaonyesha mshikamano katika wakati huu wa kihistoria , kusikiliza hofu yao na kuwahakikishia msaada wa Umoja wa Mataifa kuhakikisha wanatimiza lengo lao la kidemokrasia.

Jopo la Umoja wa Mataifa la wataalamu wa uchaguzi tayari lipo Tunisia na amewahahakikishia Watuniasia kwamba Umoja wa Mataifa uko tayari kuongeza msaada endapo utaombwa.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

"Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada wowote kwa serikali na watu wa Tunisia hususan kwenye masuala ya mchakato wa uchaguzi na mswaada wa katiba, pia kusaidia serikali ya Tunisia kurejesha utawala wa sheria na kuchagiza haki za binadamu, usawa wa kijinsia. Hiyo ni misingi muhimu ya mikataba ya Umoja wa Mataifa ambayo nimekuwa nikiifanyika kazi kwa karibu na nchi wanachama."