WFP yaunga mkono msaada kwa waathirika wa tetemeko Japan

22 Machi 2011

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP limezindua oparesheni kuisaidia serikali ya Japan kusafirisha misaada kwa waathiriwa wa tetemeko kubwa la ardhi , tsunami na milipuko ya kinu cha nyuklia nchini humo.

Mkurugezi wa WFP Josette Sheeran anasema kuwa oparesheni hiyo inafanyika kufuata ombi kutoka kwa serikali kusaidia matatizo inayokumbana nayo inapoendesha shughuli za uokoaji. Wataalamu hao wa masuala ya usafirishaji wa Umoja wa Mataifa wanasaidia kusafirisha misaada kwenye maeneo yaliyoathirika ambapo takriban watu 350,000 wanaripotiwa kuishi.

Karibu ya nusu ya fedha zinazotumika kwenye oparesheni hiyo zilitolewa na WFP , Shirika la msalaba mwekundu nchini marekani pamoja na wahisani.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter