Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia zawafungisha virago wahamiaji Ivory Coast

Ghasia zawafungisha virago wahamiaji Ivory Coast

Wenyeji wa mji mkuu wa Ivory Coast Abidjan kwa sasa wanajaribu kutumia kila mbinu kukimbia ghasia zinazoendelea kuongezeka nchini humo.

Wafanyikazi wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM mjini Abidjan wanasema watu wanaukimbia mji huo wakitumia mabasi na magari madogo ya kukodisha ili wapate kufika kwao vijijini. IOM linasema kuwa takriban wahamiaji 100,000 waliokwama watahitaji kusafirishwa nyumbani.

IOM pia limawaondoa wafanyikazi wake kutoka sehemu za magharibi mwa nchi kutokana na ukosefu wa usalama. Jemin Pandya ni msemaji wa IOM:

(SAUTI YA JEMINI PANDYA)