Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali yazidi kuwa mbaya nchini Bahrain:UM

Hali yazidi kuwa mbaya nchini Bahrain:UM

Huku hali ikiendelea kuwa mbaya nchini Bahrain watu zaidi wanaripotiwa kutoweka huku kati ya watu 50 na 100 wakiwa hawajulikani waliko kwa muda wa wiki moja iliyopita.

Watu wawili ambao awali walikuwa wametangazwa kukosekana wamepatikana wakiwa wameuawa. Ripoti zaidi pia zinasema kuwa wale waliozungumza kupitia kwa vyombo vya habari wamekamatwa na kutishwa huku wengine wakihofia usalama wao.

Kati ya waliokamatwa ni pamoja na wanaharakati wa kisiasa , watetesi wa haki za kibinadamu , madkatari na wauguzi. Rupert Colville ni kutoka ofisi ya  haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)