Hatua zahitajika kusaidia hali ya kibinadamu Lampedusa:

22 Machi 2011

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linatoa wito kwa serikali ya Italia kusaidia kupunguza msongamano ulio katika kisiwa cha Lampedusa.

Hali kwa watu 5000 wengi wahamiaji kutoka Tunisia inatajwa kuwa mbaya zaidi. Huku idadi ya wahamiaji na wenyeji wa kisiwa hicho ikiwa sawa msongamano huo umezua wasiwasi baina ya wenyeji na pia wahamiaji . George Njogopa anaripoti:

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Wakazi wa eneo hilo sasa wameanza kuingiwa na hofu kubwa na tayari serikali ya Italy imetolewa mwito kuzidisha idadi ya misafara ili kupunguza msungamano wa watu kwenye kisiwa hicho cha Lampedusa. Eneo hilo linauwezo wa kubeba watu 850 kwa wakati mmoja, lakini kwa hivi sasa idadi hiyo imepindukia hadi kufikia kiasi cha watu 2,000.

Kiasi kingine cha watu 3,000 kimeripotiwa kupata hiafadhi katika maeneo yanayotajwa kuwa ni ya hovyo

hovyo yaliyopo karibu na kituo hicho. Kutokana na hali ya hewa mbaya inayoambatana na mvua na hali ya baridi  kumewafanya wengi wao kupata shida kubwa wakati wa kusaka hifadhi.Kuna wasiwasi  mkubwa kuwepo uwezekano wa kulipuka kwa magonjwa ya kuhara.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter