Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya Walibya wakimbia makwao wakitawanyishwa na machafuko:UNHCR

Maelfu ya Walibya wakimbia makwao wakitawanyishwa na machafuko:UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa wanaoikimbia Libya na kuvuka mpaka wanasema maelfu ya watu wamekimbia makwao mashariki mwa nchi na kuchukua hifadhi kwenye mashule na kumbi za vyuo.

UNHCR inasema kuwa kuna uhaba wa madawa na mahitaji mengine katika maeneo ya mashariki mwa Libya huku bei ya bidhaa ilkipanda. Wale walio kwenye mpaka kati ya Libya na Misri waliiambia UNHCR kuwa wanaohofia kushambuliwa na wafuasi wa serikali mashariki mwa nchi.

Hadi sasa watu zaidi ya 323,000 wameikimbia libya wakielekea Tunisia, Niger na Algeria. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)