Ban aitaka Misri kutekeleza matakwa yanayotegemewa na nchi za Kiarabu

21 Machi 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitaka Misri kushikilia kipindi cha mpito kwa umakini mkubwa kwa kuhakikisha kwamba mageuzi yake yanatekelezwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na uhuru wa kweli.

Amegusia uchaguzi mkuu ujao akisema kuwa lazima wimbi la mabadiliko linafanyika sasa liharakishwe ili kukaribisha uchaguzi mkuu utakaofanyika katika mazingira ya uhuru na ukweli

Katika ziara yake ya kwanza nchini humo tangu kiongozi wa nchi hiyo Hosni Mubarak aondolewe madarakani kwa nguvu ya umma, Ban amewakikishia wananchi wa nchi hiyo kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuwa bega kwa bega hasa katika kipindi hiki alichokiita ni kigumu kwao.

Katibu Mkuu huyo amefanya mazungumzo na maafisa kadhaa wa ngazi za juu akiwemo Waziri wa mambo ya nje, Nabil el-Araby na anatazamiwa kukutana na

Waziri Mkuu Ezzad Sharaf na baadaye kukutana na baraza la kijeshi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter