Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukuaji miji Afrika unaathiri maji na usafi:UNEP

Ukuaji miji Afrika unaathiri maji na usafi:UNEP

Ukuaji wa haraka wa miji katika miongo mitano iliyopita barani Afrika unabadili sura ya bara hilo na pia kuleta changamoto kwa usambazaji wa maji na huduma za usafi imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP iliyotolewa leo.

Kwa mujibu wa tathimini ya haraka ya UNEP na shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT, miji barani Afrika inakuwa kwa haraka kuliko sehemu nyingine yoyote duniani. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

Leo hii asilimia 40 ya watu bilioni moja barani Afrika wanaishi mijini huku asilimia 60 kati yao wakiishi kwenye sehemu za mabanda ambapo kuna mazingira mabaya na uhaba mkubwa wa maji. Idadi ya watu barani Afrika wasio na maji safi ya kunywa iliongezeka kutoka watu milioni 30 mwaka 1990 hadi watu milioni 55 mwaka 2008.

wakati huo huo na muda sawia na huo idadi ya watu wasio na mazingira safi iliongezeka maradufu hadi watu milioni 175 kulingana na ripoti hiyo. Mkurugenzi wa shirika la makaazi la Umoja wa Mataifa UN-HABITAT Joan Clos hata hivyo anasema kuwa bara la afrika ndilo lililo na miji inayokua kwa haraka zaidi duniani na mahitaji ya maji na masula ya mengine ya usafi wa mazingira yanendelea kuwa machache kwenye miji hiyo