Skip to main content

Matatizo ya mionzi Japana hayajapata suluhu:IAEA

Matatizo ya mionzi Japana hayajapata suluhu:IAEA

Shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA limekuwa na kikao maalumu cha bodi ya wakurugenzi kutathimini suala la kuvuja na kusambaa kwa mionzi ya nyuklia nchini Japan.

Katika kikao hicho mkurugenzi mkuu wa IAEA Yukiya Amano amesema matatizo ya nyuklia Japan bado hayajapata suluhu na hali ya kinu cha nyuklia cha Fukushima Daiichi bado ni mbaya.

Amesema sasa imebainika kiwango kikubwa cha mionzi iliyosambaa kwenye mtambo huo na anaelewa hofu waliyonayo mamilioni ya watu kuhusu athari zake.

(SAUTI YA YUKIYA AMANO)