Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya lazima itekeleze azimio la baraza la usalama:UM

Libya lazima itekeleze azimio la baraza la usalama:UM

Wakati Uingereza, Ufaransa na Marekani wakiendelea na mashambulizi ya makombora dhidi ya maeneo na serikali ya Muammar Qadhafi wa Libya kwa nia ya kuetekeleza azimio la baraza la usalama la vikwazo vya anga nchini humo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amerejea wito wake wa serikali ya Libya kutekeleza azimio la baraza la usalama.

Ban ambaye yuko ziarani Afrika ya Kaskazini amesema Libya ni lazima iache mara moja mauaji ya raia wake na kuzingatia azimio namba 1970 na 1973 mara moja.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ameonya kwamba maisha ya maelfu ya raia yatakuwa hatarini huku janga la kibinadamu likinukia nchini humo, amesisitiza kwamba jumuiya ya kimataifa ni lazima iwe na sauti moja ili kutekeleza maazimio ya baraza la usalama.