Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aionya Syria juu ya mauaji ya waandamanaji

Ban aionya Syria juu ya mauaji ya waandamanaji

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anatia hofu na taarifa za mauaji ya waandamanaji hii leo kwenye mji wa Der\'a nchini Syria.

Ban amesema matumizi ya nguvu na kamatakamata dhidi ya wanaofanya maandamano ya amani ni vitendo visivyokubalika. Ameitaka serikali ya Syria kuachana na ghasia na kutekeleza wajibu wake wa kimataifa wa utekelezaji wa haki za binadamu ambao unahitaji kuhakikisha watu wanapata uhuru wa maoni, kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kukusanyika kwa amani.

Ban amesema kama kulivyo kwingineko ni wajibu wa serikali ya Syria kusikiliza matakwa ya watu wake na kuyashughulikia kwa kutumia majadiliano ya kisiasa yanayojumuisha wote na kuleta mabadiliko na sio ukandamizaji.