Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Natumai uchguzi wa Jumapili Haiti utafanyika kwa amani:Ban

Natumai uchguzi wa Jumapili Haiti utafanyika kwa amani:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anatumai uchuguzi wa duru ya pili wa Rais na wabunge nchini Haiti utafanyika kwa amani na utulivu.

Ameongeza kuwa uchaguzi huo wa Jumapili Machi 20 anaamini utawafanya watu wa Haitu kutumia fursa hiyo ya kihistoria ili kutanabahi mustakhbali wa taifa lao.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutolea wito uongozi wa Haiti,wagombea, wafuasi wao na umma wa nchi hiyo kuhakikisha kwamba uchaguzi wa kesho Jumapili unaleta utulivu wa kisiasa ambao nchi hiyo inahitaji ili kurejea katika maisha ya kawaida, ujenzi mpya na maendeleo.