Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waandamanaji 30 wauawa nchini Yemen:

Waandamanaji 30 wauawa nchini Yemen:

Maandamano ya amani yaliyokuwa yakifanyika nchini Yemeni yamegeuka kuwa ya ghasia na mauaji na Umoja wa Mataifa umeitaka serikali kusitisha ghasia.

Watu takribani 30 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa wakati majeshi ya usalama ya Yemen yalipowafyatulia risasi maelfu ya waandamanaji mjini Sanaa.

Martin Nersiky msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Ban Ki-moon anasikitishwa sana na hali ya machafuko inayoendelea Yemen na ametoa wito kwa pande zote kujizuia huku akiikumbusha serikali ya Yemen kwamba ina wajibu wa kuwalinda raia.

Maandamano yamekuwa yakiendelea Yemen kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa, watu wakimtaka Rais ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo mitatu sasa kujiuzulu. Lakini Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh amesema atang'atuka tuu pale muhula wake utakapomalizika 2013.