Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyombo vya sheria vinapaswa kuwasaidia wanawake kupata haki zao:UM

Vyombo vya sheria vinapaswa kuwasaidia wanawake kupata haki zao:UM

Umoja wa Mataifa kwa kupitia mashirika mbalimbali likiwemo la idadi ya watu duniani UNFPA, la watoto UNICEF, la maendeleo UNDP na sasa kitengo kipya cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia masuala ya wanawake UN-Women imekuwa msitari wa mbele kuchagiza serikali kuhakikisha haki za wanawake zinalindwa.

Miongoni mwa haki hizo ni za urithi, haki za elimu, kiuchumi, kisiasa na kijamii, na moja ya njia ambazo wanawake wanahimizwa kuzifuata ni kutumia sheria. Nchi mbalimbali hasa za Afrika ya Mashariki zimekuwa zikifania marekebisho ya katiba zao kuhakikisha mwanamke anakuwa na sauti na kuwezeshwa katika jamii.

Kwa ushirikiano na mshirika mbalimbali ya kisheria yanayopigania wanawake na makundi ya wanaharakati, wanaelimisha na kuhamasisha jamii kuhsu haki za wanawake.

Nchini Kenya FIDA shirika ambalo ni la mawakili wanawake limejitoa kimasomaso kuwasaidia wanawake, mwandishi wetu mjini Nairobi Jason Nyakundi alifika kwenye ofisi za FIDA na kukutana na wakili Bi Jane Serwanga aliyemfahamisha nini wanachokifanya kumsaidia mwanamke wa Kenya kisheria, Wasikilize.

(MAHOJIANO NA JANE SERONGA)