Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jitokezeni kupiga kura yasema MINUSTAH Haiti

Jitokezeni kupiga kura yasema MINUSTAH Haiti

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti umesema kuwa kuwepo kwa utulivu wa kisiasa na kukua kwa uchumi wa nchi hiyo kunategemea kwa upande mwingine idadi kubwa ya watu watakaojitokeza kupiga kura wakati wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki.

Ujumbe huo ujulikanao kama MINUSTAH unasema kuwa ikiwa wapiga kura wengi watajitokeza wananchi wa Haiti wataonyesha umuhimu wa shughuli hiyo na moyo wa kuwachagua viongozi wanaowaamini.

Aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa Haiti Mirlande Manigat na mwanamuziki maarufu Michel Martelly wanawania kiti cha urais kwenye duru ya pili ya uchaguzi miezi minne baada ya kuandaliwa kwa dura ya kwanza.

Kwa upande mwingine akiwa ziarani nchini Guatemala juma hili Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa shughuli za kuijenga upya Haiti mwaka mmoja baada ya kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi zinashika kasi huku pia maradhi ya kipindupindu yakidhibitiwa.