Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanaoishi makambini Haiti inapungua:IOM

Idadi ya wanaoishi makambini Haiti inapungua:IOM

Idadi ya watu wanaoishi kwenye kambi nchini Haiti baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi lililowaacha wengi bila makao inaendelea kupungua kwa kiasi kikubwa.

Inaripotiwa kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani wanaosalia kwenye kambi ni chini ya nusu ya wakimbizi wote waliokuwa kwenye kambi kulipotokea tetemeko hilo. Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na usimamizi wa kambi unakadiria kuwa hadi sasa kuna wakimbizi 680,000 kambini.

 IOM na ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti wanasema kuwa kati ya sababu ambazo zimefanya kuendelea kuhama kwa idadi kubwa ya watu ni pamoja na ukosefu wa salama , kuendelea kuzorota kwa hali ya usafi na kupatikana kwa makao ya kudumu.