Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuchelewa kwa hatua kunaweza kuvuruga amani Sudan:UM

Kuchelewa kwa hatua kunaweza kuvuruga amani Sudan:UM

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa Mohamed Chande Othman amesema hali ilivyo katika jimbo la Abyei ni ya kuvunja moyo kutokana na kuendelea kujiri kwa matukio ya uvunjifu wa amani ambayo yanaweza kuvuruga juhudi za kuleta amani kwa Sudan nzima.

Amesema hali ya wasiwasi inazidi kumea mizizi kutokana na ucheleweshaji wa zoezi la upigaji wa kura ya maoni kwa jimbo hilo huku kukiwa na taarifa kwamba baadhi ya wakazi wa jimbo hilo la Abyei ambao walisafiri hadi Sudan Kusini kwa ajili ya upigaji wa kura ya maoni miezi miwili iliyopita wamepigwa marafuku kufanya misafara.

Mtaalamu huyo wa masuala ya haki za binadamu ameonya kwamba kuchelewa utekelezaji wa maazimio muhimu ni kitisho kwa usalama wa eneo hilo ambalo limeshuhudia migogoro ya wenyewe kwa wenyewe kwa miongo kadhaa.

Jaji Chande Othman ambaye amekamilisha ziara yake kwenye maeneo mbalimbali nchini Sudan ametaka kufanyika kwa juhudi za makusudi kukamilisha baadhi ya maeneo yaliyosalia kama ilivyouanishwa kwenye  mkataba wa amani wa mwaka 2005. Kazi ya kuwaokoa raia wa Mauritania walioko Ivory Coast kuendelea licha ya kuzuka machafuko