Misitu ni muhimu kutatua tatizo la maji:FAO

Misitu ni muhimu kutatua tatizo la maji:FAO

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO leo limeonya kwamba ifikapo mwaka 2025 watu bilioni 1.8 watakuwa wakiishi kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa wa maji na theluthi mbili ya watu wote duniani watakabiliwa na matatizo ya maji .

FAO imesema misitu ni muhimu kwani inaweza kupokea na kuhifadhi maji na itakuwa na jukumu kubwa katika kupatikana kwa maji ya kunywa kwa mamilioni ya watu katika miji mikubwa duniani.

Kufuatia hali hii ushirikiano wa wadau wa misitu CPF na mashirika ya kimataifa yanayojihusisha na misitu yametoa wito kwa nchi zote duniani kutoa kipaumbele katika kufifadhi na kulinda misitu kwa ajili ya kunusuru tatizo la maji.