Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa haki za binadamu amelaani mauaji ya raia Ivory Coast

Mkuu wa haki za binadamu amelaani mauaji ya raia Ivory Coast

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea hofu juu ya kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Ivory Coast. Amesema mashambulizi dhidi ya raia hayakubaliki na kulaani mauaji ya jana kwenye kitongoji cha Abobo mjini Abidjan ambako makombora yamekatili maisha ya watu takriban 30 na kujeruhi wengine wengi.

Amesema mashambulizi hayo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa kama anavyofafanua msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Rupert Colville.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Kwa upande wake shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema maelfu ya watu wanaohitaji msaada wanashindwa kufikiwa kutokana na usalama mdogo na limetoa wito wa kuruhusu wafanyakazi wa misaada kuweza kufanya shughuli zao.

UNHCR inasema watu zaidi wanakimbilia nchi jirani ya Ivory Coast sasa idadi yao ni 90,000 na inatarajiwa kufika 100,000, na Jumamosi wiki hii inaanza kuwahamisha wakimbizi wa Liberia 24,000 wanaathirika na mapigano nchini Ivory Coast.