Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya yasema itatekeleza azimio la baraza la usalama 1973

Libya yasema itatekeleza azimio la baraza la usalama 1973

Baada ya azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa namba 1973 lililopitishwa jana usiku likimtaka kanali Muammar Qadhafi kutekeleza mara moja usitishaji wa mapigano na likimuwekea vikwazo vya safari za anga kuzuia utawala wake kutumia nguvu za anga dhidi ya watu wa Libya, leo serikali ya Libya imetangaza kusitisha mapigano mara moja na operesheni zote za kijeshi.

Akizungumza kupitia televisheni ya taifa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Musa Kusa amesema usitishaji huo wa mapigano una lengo la kuwalinda raia. Wakati huohuo hali ya kibinadamu imeelezewa kuzidi kutia hofu hasa maeneo ambayo mapigano bado yanaendelea, huku mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos akitiwa hofu na matumizi ya silaha na mabomu dhidi ya raia.

Ameonya kwamba kutakuwa na athari kubwa kwenye mji wa Benghazi na amezitaka pande zote kuchukua hatua za kuwalinda raia.