Skip to main content

Baraza la usalama la UM limeiwekea Libya vikwazo vya safari za anga

Baraza la usalama la UM limeiwekea Libya vikwazo vya safari za anga

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuiwekea vikwazi vya anga Libya ili kuzuia majeshi ya anga ya nchi hiyo kushambulia raia.

Azimio hilo limetoa witowa kupigwa marufuku safari zote ndege kwenye anga ya Libya isipokuwa tuu zile mza kupeleka misaada ya kibinadamu.Baraza limewaidhinisha nchi wanachama kuchukua hatua zote za lazima kuhakikisha marufuku hiyo na kushirikiana na Umoja wa Mataifa kwa hatua zozote zitakazochukuliwa kutekeleza marufuku hiyo.

Azimio hilo pia limejumuisha vikwazo vya silaha na vya kuchumi lakini limeondoka vile vya kukaliwa kwa nguvu.Baadhi ya nchi za Kiarabu na za Afrika pamoja na Marekani, Ufaransa na Uingereza wameshinikiza kuchukuliwa kwa hatua hiyo.Balozi wa Uingereza kwenye Umoja wa Mataifa Mark Lyall Grant anasema

(SAUTI YA MARK LYALL GRANT)

Azimio namba 1973 linataka kanali Muammar Qadhafi kutekeleza mara moja usitishaji wa mapigano. Linaweke vikwazo vya safari za anga kuzuia utawala wa Qadhafi kutumia nguvu za anga dhidi ya watu wa Libya. Linaidhinisha nchi wanachama kuchukua hatua zote za lazima kuwalinda raia na maeneo ya raia yaliyoko kwenye tisho la kushambuliwa.

Limepinga kuingiliwa na majeshi ya nje kwa mfumo wowote kwenye himaya ya Libya, pia limeweka hatua zingine zikiwemo kuimarisha vikwazo vya silaha na kuunyima utawala fursa ya kupata fedha. Azimio hilo limepitishwa Alhamisi usimu kwa kura 10 za kuunga mkono na wajumbe watano hawakupiga kura wakiwemo Brazil, China, Ujerumani , India, na Urusi.