Afghanistan itaendelea kuhitaji msaada wa kimataifa

17 Machi 2011

Afghanistan inahitaji msaada wa kimataifa unaoendelea kama kweli inataka kuchukua majukumu ya nchi hiyo Machi 21 amesema balozi wa Afghanistan kwenye Umoja wa Mataifa Zahir Tanin.

Balozi Tanin ameyasema hayo leo kwenye baraza la usalama lililokuwa likijadili taifa hilo la Asia ambalo linakabiliwa na tishio kubwa la wanamgambo wa Taliban na ambalo limekuwa likisaidiwa na majeshi ya kimataifa kurejesha usalama.

Balozi huyo ameongeza kwamba viongozi wa Afghanistan pia wanahofia makampuni binafsi ya usalama yanayoendesha shughuli zake nchini humo

(SAUTI YA ZAHIR TANIN)

Wakati tukijiandaa kuanza rasmi mchakato wa kipindi cha mpito hapo Machi 21, tunauchukulia Umoja wa Mataifa kama mshirika mkuu wa kufanikisha hili. Afghanistan haiwezi kusimama peke yake endapo taasisi za serikali zitaendelea kutokuwa imara na kuingiliwa na mifumo mengine na pia kama uwezo wake hautoimarishwa.

Balozi Tanin amesema kwamba katika miaka mine ijayo jukumu la jumuiya ya kimataifa nchini Afghanistan litakuwa ni kushughulikia mahitaji ya mchakato wa kipindi cha mpito.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter