Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wajadili hali ya Haiti ikijiandaa kufanya uchaguzi

UM wajadili hali ya Haiti ikijiandaa kufanya uchaguzi

Umoja wa Mataifa umewataka wagombea wa uchaguzi nchini Haiti hususan wa kiti cha Urais kuacha kutoa matamshi ya kushambulia pamoja na vitisho huku ghasia zinazoambatana na kampeni zikiendelea kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi siku ya Jumapili.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUSTAH unasema kuwepo kwa demokrasia nchini Haiti kunategemea jinsi wanasiasa watakavyochangia katika kubadilishana madaraka na kukubali matokeo ya uchaguzi.

Aliyekuwa mke wa rais wa zamani nchini Haiti Mirlande Manigat na mwanamuziki maarufu Michel Martelly wanawania kiti cha uaris kwenye uchaguzi uliohairishwa kwa miezi miwili kufuatia kutokea kwa ghasia baada ya matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais kutangazwa mwezi Disemba .