Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtangazaji wa Canada awa balozi wa WFP dhidi ya njaa

Mtangazaji wa Canada awa balozi wa WFP dhidi ya njaa

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mpango wa chakula WFP imemwidhinisha mtangazaji wa zamani kutoka Canada George Stroumboulopoulos kuwa balozi wake wa masuala ya njaa.

Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya mtangazaji huyo wa zamani kuwasili akitokea nchini Pakistan ambako WFP imekuwa ikiwalisha mamia ya raia wanaoanza upya ujenzi wa maisha yao kufuatia kuharibiwa na mafuriko.

Akizungumza na wasikilizaji wake kwenye kituo cha redio kimoja CBC, Stroumboulopoulos amezungumzia umuhimu wa kuendelea kuwakumbuka raia wa eneo hilo akisema kuwa suala la kufikiwa na huduma muhimu kama chakula siyo nanga ya kisiasa wala mashirikiano na jukumu la kutambua kuwa wananchi hao wanahitaji msaada.

Pia amesifu juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na WFP kuwafikia watu wenye mahitaji duniani kote,ikiwemo harakati zake za kukabiliana na tatizo la njaa.