Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahitimisha ziara Guatemala na anaelekea Afrika Kaskazini

Ban ahitimisha ziara Guatemala na anaelekea Afrika Kaskazini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amejadili na viongozi wa amerika ya Kati kuhusu hali inayoendelea katika ulimwengu wa Kiarabu na Afrika ya Kaskazini hususan Libya.

Ban aliyekuwa ziarani nchini Guetemala amesisitiza kwamba viongozi wa nchi za Kiarabu lazima wasikilize sauti za watu wao. Ameongeza kuwa hakuna nafasi kwa ajili ya ghasia na matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya raia ni uhalifu dhidi ya ubinadamu chini ya sheria za kimataifa.

Ban amesema wale wote wanaohusika watawajibishwa. Pia katika mazungumzo na viongozi wa Guatemala Ban wamegusia suala la Haiti na juhudi za serikali za America ya Kati kutekeleza demokrasia. Ban anaondoka Guatemala na kuelekea Afrika ya Kaskazini atakakozuru Tunisia na Misri.