Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala kuhusu haki ya ardhi kwa watu wa asili ni muhimu:UM

Mjadala kuhusu haki ya ardhi kwa watu wa asili ni muhimu:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili James Anaya ametoa wito wa mawasiliano zaidi baina ya serikali, watu wa asili na makabila huko Surinam na kuahidi kuendelea kusaidia juhudi za haki za watu hao za kumiliki ardhi na rasilimali zingine.

Amesema anatarajia kuwa na mazungumzo na pande zote husika Suriname ili kuhakikisha kunatolewa muongozo wa hatua za kuchukuliwa kuweza kufanikisha kupatikana haki za ardhi za watu wa kikabila na wa asili kwa kuzingatia mikataba ya kimataifa ambayo Suriname imeiridhia.

Ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara yake ambayo ni ya kwanza kufanywa na mtaalamu aliteuliwa na baraza la haki za binadamu. Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)