Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maambukizi ya HIV kutoka kwa mama hadi kwa mtoto kudhibitiwa

Maambukizi ya HIV kutoka kwa mama hadi kwa mtoto kudhibitiwa

Wadau muhimu wanaojihusisha na masuala ya HIV na ukimwi wamekubaliana njia muafaka ya kusaidia kutokomeza maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Mpango huo mpya wa kikanda umeidhinishwa leo mjini Nairobi Kenya wakati wa hitiomisho la mjadiliano ya siku tatu yaliyohusisha washiriki kutoka shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, shirika la afya duniani WHO, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDS na wadau wengine.

Pia mjadala huo ulihudhuriwa na wawakilishi wan chi 15 zilizoathirika sana na ukimwi, jumuiya za kijamii na wahisani mbalimbali. UNICEF inasema watoto 370,000 bado wanaambukizwa virusi kwa mujibu wa takwimu za 2009 lakini sasa ni wakati wa kuleta mabadiliko, na limeongeza kuwa inawezekana kuwa na kizazi bila ukimwi ifikapo 2015.