Skip to main content

Baraza la usalama lajadili vikwazo dhidi ya Libya

Baraza la usalama lajadili vikwazo dhidi ya Libya

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limeendelea na mjadala kuhusu azimio la kuiwekea vikwazo Libya.

Kwa mujibu wa balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice mjadala wao unagusia hatua mbalimbali za kuchukuliwa ili kuwalinda raia na kuongeza shinikizo kwa utawala wa Muammar Qadhafi kuacha mauaji na kuruhusu watu wa Libya kujieleza na kutanabaisha matarajio yao ya baadaye kwa amani na uhuru.

Amesema pia katika mjadala huo utakaoendelea leo suala la vikwazo vya anga litaangaliwa na athari zake kwa raia na pia nafasi ya jumuiya ya nchi za kiarabu ni muhimu sana kwa ajili ya suluhu ya Libya.

(SAUTI YA SUSAN RICE)