Skip to main content

UM hofia jeshi kushikilia hospitali Bahrain

UM hofia jeshi kushikilia hospitali Bahrain

Majeshi ya usalama nchini Bahrain yameteka kwa nguvu hospitali kadhaa na vituo vya afya kwa mujibu wa ofosi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Katika mji mkuu Manama majeshi yamearifiwa kuwafanyia ghasia wahudumu wa afya na kuwazuia wafanyakazi na wagonjwa kuingia au kutoka katika hospitali ya mji huo na umeme umekatwa hospitalini hapo.

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema uvamizi wa hospitali hiyo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na ameukumbusha uongozi wa Bahran kuwa una wajibu wa kulinda haki ya kuishi na ya afya kwa raia wake.Ravina Shamdasani ni kutoka ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA RAVINA SHAMDASAN)

Kamishina mkuu amesema kuendelea kwa ghasia Bahrain hakukubaliki na ametoa wito wa kuwepo mazungumzo kati ya serikali na makundi ya upinzani ili kumaliza mzozo na kuleta mabadiliko. Amesema kutangazwa kwa hali ya tahadhari kulikofanyika hivi karibuni kusitumike kama sababu ya kuwanyima raia wa Bahrain haki ya uhuru wanaostahili.