Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO imeonya juu ya matumizi ya potassium iodide Japan

WHO imeonya juu ya matumizi ya potassium iodide Japan

Shirika la afya duniani WHO leo limeouonya umma wa Japan juu ya matumizi ya madini ya potassium iodide au bidhaa zenye iodide kama njia ya kujikinga na mionzi ya nyuklia.

Ushauri huo umefuatia taarifa kwamba watu nchini Japan na kwingineko wanatumia madini ya potassium kujikinga na mionzi inayosambaa kutoka kwenye mtambo wa nyuklia nchini humo. WHO inasema madini hayo yatumike tuu pale ambapo imeshauriwa kufanyika hivyo kwa kunusuru afya ya jamii.

Limesema matumizi yasiyo salama ya madini hayo yanaweza kuleta athari kubwa kama kuleta kichefuchefu, kupata vipele, matatizo ya tumbo na uwezekano mkubwa kwa kuzurika na madini hayo. Shirika hilo limesema vidonge vya potassium iodide mtu akipewa kabla au muda mfupi baada ya kupatwa na mionzi ya nyuklia inaweza kusaidia kuzuia saratani lakini hazimzuii mtu kupatwa na mionzi.