Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udhibiti wa kusambaa kwa mionzi unaendelea Japan:IAEA

Udhibiti wa kusambaa kwa mionzi unaendelea Japan:IAEA

Shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA limethibitisha kwamba jeshi la Japan limefanya awamu nne za kumwaga maji kwenye kwa njia ya helkopta kwenye jengo lenye mtambo wa tatu wa kinu cha nyuklia cha Fukushima Daiichi.

IAEA imeongeza kuwa mtambo huo ulilipuka na kujeruhi watu 52 na 17 wanapata tiba baada ya kuathirika na mionzi ya nyuklia.  Wakati huohuo theluji inayoendelea kumwagika nchini Japan imeongeza ugumu katika shughuli za misaada kwa mamilioni ya waathirika wa tetemeko na tsunami.

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema na hofu inaongezeka juu ya wale ambao hadi sasa hawajafikiwa na waokozi au watoa misaada na watu wengine 500,000 ambao wanaishi kwenye vituo hivi sasa, wengi hawana nguo za baridi.

Hofu ya mionzi imeongeza tahamki miongoni mwa watu wanaohisi hawapati taarifa za kutosha kama anavyofafanua mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Tokyo Mari Yamashita.

(SAUTI YA MARI YAMASHITA)

Hadi sasa watu zaidi ya 5000 wamethibitishwa kufa na wengine zaidi ya 10,000 hawajulikani walipo, na idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka.