Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanasoka Stoitchkov yuko Burkina Faso kuunga mkono juhudi za EU na FAO

Mwanasoka Stoitchkov yuko Burkina Faso kuunga mkono juhudi za EU na FAO

Mwanasoka nyota wa Bulgaria Hristo Stoitchkov amezungumzia utayari wake wa kuunga mkono mpango unaondeshwa na umoja wa ulaya na shirika la kimataifa la chakula na kilimo FAO wenye lengo la kuwasaidia mamia ya wananchi ambao waliathiriwa na baa la ukosefu wa chakula huko Sahel.

Akiwa kwenye ziara ya siku mbili nchini Burkina Faso pamoja na ujumbe mwingine wa wanasoka toka chama cha wanasoka wa kulipwa barani ulaya, mwanasoka huyo alitembelea miradi inayoratibiwa na mashirika hayo ambayo hadi sasa imewafaidia familia nyingi zilizokosa chakula kutokana na hali ya ukame iliyokumba eneo hilo mwaka 2010.

 

Mwasoka huyo amesema kuwa ni jambo la muhimu kuwawezesha wale wote waliathiriwa na hali hiyo na njia ya muhimu zaidi ni kuwajali na chakula

 

Katika maisha yake ya soka amepata kupata mafanikio makubwa zaidi wakati akiwa na klabu yake ya Barcelona katika mwaka 1990 na ndipo alipounga mkono miradi inayoendeshwa na mashirika ya kimataifa.

 

Nchini  Burkina Faso, FAO hupokea kiasi cha pound million 1.8 kutoka kwa jumuiya ya umoja wa ulaya kwa ajili ya kugharimia kuendeleza mifugo na uendelezaji wa bustani katika maeneo ya mijini