Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande hasimu nchini Libya zatakiwa kusitisha mapigano

Pande hasimu nchini Libya zatakiwa kusitisha mapigano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amezitaka pande zilizo kwenye vita nchini Libya kukukubali kusitisha mapigano hayo.

Ban alionya kuwa wale wote wanaotumia wanajeshi kuwashambulia raia watachukuliwa hatua za kisheria. Wito huo wa Ban unajiri wakati ambapo wanajeshi wa Libya wanapoendelea kuwashambulia waasi yakiwemo mashambulizi ya angani. Ban ameongezea kuwa mashambulizi kwenye miji kwa mfano mji wa Benghazi kunayaweka hatarini maisha ya raia. Ban amezitaka pande husika kusitisha mapigano na kuheshimu azimio la Umoja wa Mataifa la 1970.