Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa wito wa kuwepo usimamizi mwema kwa mali ghafi ya Afrika

UM watoa wito wa kuwepo usimamizi mwema kwa mali ghafi ya Afrika

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa serikali za Afrika ni lazima ziwajibike kuhakikisha kuwa mali ghafi yaliyo kwenye bara hilo yakiwemo mafuta yanachangia katika ukuaji wa uchumi wa bara hilo.

Mkurugenzi mkuu wa  shirika la maendeleo ya kiviwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO Kandeh Yumkella anasema kuwa viongozi wa nchi za Kiafrika ni lazima wawe na maono na mipango bora. Akiongea mjini Accra Ghana Yumkella anataka ajenda ya maendeleo kupewa kipau mbele kwa miaka 20 inayokuja ili kuziwezesha nchi za bara la Afrika kutotegemea tu mafuta na gesi.

Yumkella amengoza kuwa nchi za Kiafrika ni lazima zihakikishe kuwa utajiri mpya hauna madhara kwa ule wa zamani kwa kuhakikisha kuwa zimejenga sekta ya kiviwanda ili kushindana na nchi zingine duniani.