Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shirika la UM la kudhibiti nishati ya atomic kutuma wataalamu nchini Japan

Shirika la UM la kudhibiti nishati ya atomic kutuma wataalamu nchini Japan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nishati ya atomic IAEA linatarajiwa kuwatamu wataalamu wake wa masuala ya mazingira nchini Japan kufuatia kulipuka kwa vinu vya kinyuklia nchini humo.

Akihutubia waandishi wa habari kwenye makao makuu ya shirika hilo mjini Vienna mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Yukiya Amano anasema kuwa ajali ya kinu cha Fukushima ni tofauti na ajali mbaya zaidi ya Chernobyl iliyotokea miaka 25 iliyopita.

Wiki moja iliyopita bwana Amano alihifamisha bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo kuwa matumzi ya nishati ya atomic duniani ni salama tangu makasa wa Chernobyl ambapo takriban watu milioni 8 katika zilizo sasa nchi ya Ukraine , Belarus na Urusi waliathiriwa na miale hatari na kupatwa na magonjwa ya saratani. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na mikasa kuanzia hapo kesho watayazuru maeneo yaliyoathirika na tetemeko ya ardhi la wiki iliyopita nchini Japan lililosababisha kutokea kwa gharika ya tsunami.