Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uturuki imetakiwa kuruhusu waandishi kufanyakazi kwa uhuru:UM

Uturuki imetakiwa kuruhusu waandishi kufanyakazi kwa uhuru:UM

Uongozi nchini Uturuki umetakiwa na Umoja wa Mataifa kuruhusu wanahabari na waandishi kufanya kazi zao kwa uhuru.

Kauli hiyo inafuatia kuwekwa rumande waandishi tisa Machi 3 mwaka huu kwa madai ya kujihusisha na kile kilichoelezwa kutaka kuipindua serikali.

Msemaji wa mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Rupert Colville amesema watu wanaoshikiliwa ni pamoja na mwandishi mashuhuri kwa kuukosoa mfumo wa sheria na jeshi la pilsi nchini Uturuki.

Ameongeza kuwa bado haijafahamika bayana endapo mahabusu hao wanachunguzwa kutokana na kazi zao kama waandishi habari na watangazaji au kuna ushahidi mwingine dhidi yao usiohusiana na kazi za uandishi.