Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Kiarabu zataka Libya iwekewe vikwazo vya anga

Nchi za Kiarabu zataka Libya iwekewe vikwazo vya anga

Nchi wanachama wa jumuiya ya kiarabu imetoa taarifa ikilitaka baraza la usalama kupitisha azimio la kupiga marafuku anga ya Libya kuruhusu ndege kuruka ili kuvidhibiti vikosi vitiifu vya Muammar Qadhafi kutumia anga hiyo kufanya mashambulizi.

Vikosi vya kiongozi wa Libya vimekuwa vikitumia anga ya eneo la nchi za kaskazini kudhibiti makundi ya waaandamanaji wanaotaka kuondosha utawala wake. Balozi wa Lebanon kwenye Umoja wa Mataifa Nawaf Salam akizungumza kwenye kikao cha baraza la usalama kinachokutana kwa faragha amesema kuwa baraza hilo linafanyia kazi azimio la kuipiga marafuku anga hiyo.

Azimio la baraza hilo lililopitishwa mapema mwezi February mwaka huu liliuwekea vikwazo utawala wa Muammar Qadhafi wa kutosafirishwa silaha