Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM na China kuwakwamuwa waathirika wa usafirishaji haramu

IOM na China kuwakwamuwa waathirika wa usafirishaji haramu

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM kwa kushirikiana na serikali ya China leo wanatazamiwa kuendesha mafunzo ya siku tatu ambayo yanalenga kuwasaidia watu waliokumbwa na vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu

Mafunzo hayo yanayofanyika mjini Beijing yanajulikana kama njia bora ya kuwasaidia waathirika wa vitendo hivyo kwa kuwaangazia na kuwakumbuka juu ya maskani bora, kuwapa ulinzi na kuwapa msaada mwingine wa hali na mali.

 

Mafunzo hayo yanawaleta pamoja mameneja wa makazi kutoka kila pande ya nchi hiyo na yamepigwa jeki na serikali ya Marekani kupitia kitengo chake cha kinachohusika na masuala ya idadi ya watu, uhamiaji na wakimbizi.

 

Katika miaka ya hivi karibuni Serikali ya China imeongeza juhudi kukabiliana na wimbi la ongezeko la usafirishaji haramu wa binadamu kwa kuanzisha kampeni za kitaifa na kubana mianya inayotumiwa na magenge ya wacheche kusafirisha binadamu.