Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasaidia wahamiaji kupata taarifa Japan

IOM yasaidia wahamiaji kupata taarifa Japan

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasaidia juhudi zinazoendelea za kusambaza taarifa kuhusu tetemeko na misaada ya dharura kwa jamii za wahamiaji zinazoeishi nchini Japan.

Kuna vyombo vingi vya habari vinavyotangaza kwa lugha mbalimbali nchi Japan vikiwemo vinavyotangaza habari kupitia shirika la serikali NHK na vyombo vingine binafsi na vya kibiashara kama Wai Wai FM ambayo inatangaza kwa lugha za Bahasa Indonesia, Bengali, Kichina, Kiingereza , Kifilipino, Kikorea, Kireno, Kihispania, Kiswahili, Urdu, Kithai na Kivietnam.

Idhaa hizi zina lengo la kutoa taarifa kwa wahamiaji wasiozungumza Kijapan ili wajue wapi pa kupata msaada wa malazi, chakula na madawa.