Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za binadamu zinaendelea kukiukwa na viongozi nchini Sudan:Jaji Mohamed Chande Othman

Haki za binadamu zinaendelea kukiukwa na viongozi nchini Sudan:Jaji Mohamed Chande Othman

Haki za binadamu nchini Sudan zinaendelea kukiukwa na viongozi wa nchi hiyo amesema mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Sudan.

Mtaalamu huyo jaji Mohamed Chande Othman kutoka nchini Tanzania ndio kwanza amerejea nyumbani baada ya kuzuru Sudan kwa siku nane, kuanzia Sudan Kusini hadi jimbo lililoghubikwa na migogoro la Darfur.

Jaji Othman amekuwa Sudan kutathimini hali ya haki za binadamu Kaskazini, Kusinini na jimbo lenye utajiri wa mafuta la Abyei.Amezungumza na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha kuhusu ziara yake ya Sudan.

(MAHOJIANO NA JAJI MOHAMED CHANDE OTHMAN)