Ban alaani matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji Yemen

14 Machi 2011

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ameelezea hofu iliyopo kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Yemen na kushutumu matumizi ya nguvu kupita kiasi na wanajeshi dhidi ya maandamano ya amani kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Sanaa ambapo watu kadha waliuawa na wengi kujeruhiwa.

Ban ameitaka serikali ya Yemen na makundi pinzani kuafikia makubaliano ili kuzuia kuendea kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo. Ban pia ameitaka serikali kuheshimu viwango vya kimataifa vya haki ya kibinadamu na kufanya uchunguzi kuhusiana na madai mauaji na ukiukaji wa haki za binadamu vinavyoendelea nchini humo.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa polisi nchini humo waliwashambulia waandamanaji kwenye mji wa Sanaa ambapo watu sita waliuawa na wengine kujeruhiwa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter